Category: Kiswahili

Zetu ni Uhamiaji au uhamishaji, biashara au bi hasara?

      Image result for photos of wachina morogoro      Taarifa kuwa kuna wachina walikamatwa wakiendesha kiwanda bila kibali nchini kwa tangu mwaka 2010 huko Morogoro ni za kuchefua na kuchukiza. Sikujua kuwa nchi yetu itafikia hapa kiasi cha kuibiwa kana kwamba ni nchi ya mataahira au marehemu kiakili. Tokana na kadhia hii, kuna maswali tunayopaswa kujiuliza kama taifa na watu wenye akili mojawapo yakiwa: Je uhamiaji hakikuwa na taarifa au walikatiwa kitu? Je kuna wachimbaji wa kigeni wangapi nchini? Je mchezo huu ulianza lini?  Pia visa vya wachina kukamatwa ima wakichimba madini au kufanya kazi na kuishi bila vibali au kutorosha nyara za umma na madini vimezidi nchini. Sijui wako wahindi, wapakistani, waturuki, wanigeria na wengine wangapi wanaofanya mambo kama haya nchini wakati wananchi wetu wakishuhudia au kuripoti mamlaka zisichukue hatua?

            Ukiachia mbali uhamiaji, ilikuwaje wizara ya madini haikujua au nao wana ushirika katika kuliibia taifa kwa kufumbia macho wezi kama hawa ili mradi wanapata chao?  Japo ni mapema kutoa lawama, kuna uwezekano huu ni mchezo wa baadhi ya maafisa wa juu nchini. Maaana, hakuna kilichonishangaza kama kusikia kuwa wachina hao waliokutwa wakihujumu nchi walikuwa wapelekwe Dar es Salaam ili warudishwe kwao. Warudishwe kwao wakasherehekee kuwaibia mataahira siyo? Kwanini warejeshwe kwao wakati wanakabiliwa na mashitaka lukuki yakiwemo ya kuhujumu uchumi na kutishia usalama wa taifa kwa kuingia na kuishi na kufanya kazi kinyemela? Je hawa wanaotaka kuwarejesha kwao kweli hawajui sheria au kuna kitu wanataka kuficha. Haiwezekani mtu avunje sheria ya nchi hata kama ni mgeni aondolewe nchini bila kuhukumiwa na mahakama nchi ikawa salama.  Hata mhalifu kama huyu akikamatwa na chizi, achia mbali mtu mwenye akili timamu, atamsulubu. Hata akikamatwa na mbwa, hataaacha lau kumng’ata kwa kujua na kutambu aanavyomhujumu. La msingi, mafisadi na wasaliti wanaokula na wahalifu hawa, ni kujua kuwa wakati wakiwaachia wachina hawa au wahalifu wa mataifa mengine, kuna vijana wengi wa kitanzania wanaozea kwenye magereza ya nchi mbali mbali hasa China wakingoja kunyongwa kwa kupatikana na hatia za kusafirisha madawa ya kulevya. Hawa nao ni watafutaji sawa na hawa wachina hata kama wanafanya uhalifu tofauti. Nadhani hapa tofauti yao ni kwamba hawa wanauza unga na hawa wanaiba raslimali za nchi. Hivi watanzania tulirogwa na nani na kuwa na roho mbaya hivi itokanayo na ujinga, upogo, ulafi na ubinafsi? Tunachezea raslimali zetu kana kwamba tutaishi milele. Hivi mababu zetu wangekuwa wapumbavu hivi tungekuta nini zaidi ya mashimo na mabwana wa kutugeuza watumwa?  Mamlaka zinazohusika na kupambana na rusha na ufisadi, zifuatilie kisa hiki zinaweza kugundua vingi na mengi hasa wakati huu ambapo jinai ya kushirikiana na wageni kuibia taifa inazidi kuwa kidonda ndugu.
            Mbali na wizara ya madini, ilikuwaje wizara ya biashara na viwanda nayo haikufahamu kama hakuna mchezo mchafu hapa?  Maana, ushahidi kuwa kuna mchezo mchafu, ni maneno ya Afisa mmoja wa madini aliyelalamika kuwa aliwahi kushughulikia sakata hili akasimamishwa kazi. Je wako wezi kama hawa wangapi nchini na wameishaliingizia taifa hasara kiasi gani? Je wapo watendaji wangapi wa serikali wako nyuma ya hujuma hii na kwa muda gani? Haiingii akilini eti kwa nchi yenye vyombo vyote vya usalama isiwe na taarifa za watu tena kutoka mbali kama China wenye rangi tofauti kwa miaka yote hii. Kama ni hivi basi Tanzania ni nchi ya ajabu na usalama wake uko hatarini.
            Pamoja na kwamba kwa sasa China inaonekana kama mwekezaji mkubwa nchini, tunapaswa kuwa makini. Kwani haina tofauti na nchi za magharibi zilizotutawala na kutunyonya kwa muda mrefu kabla ya mababu zetu kujitoa mhanga kupigania uhuru. Tofauti na nchi za magharibi zilizokuwa zikituma vikundi vichache vya mawakala wao kama vile wamisionari, wafanyabiashara, wavumbuzi na watawala, wachina wanatutumia watu wao wasio na ajira kuja kuchukua ajira za watu wetu ukiachia mbali kujiingiza kwenye shughuli za jinai baada ya kubaini kuwa baadhi ya watendaji wetu ni walafi na wapumbavu wasio na mapenzi na taifa lao. Huu upuuzi unaoripotiwa kila siku huwezi kuutenda China ukaachiwa uende kwenu. Watakupiga risasi. Ni bahati mbaya kuwa kosa la kuhujumu uchumi au ufisadi nchini linafanyiwa mchezo tokana na kuhusisha wakubwa wengi. Kule China wanapiga risasi bila kujali wewe ni rais, raia au mgeni.
            Tumalizie kwa kuzitaka mamlaka kuchunguza aina hii ya ufisadi na uhujumu kwa taifa. Pia tunashauri zitungwe sheria kali za kupambana na wezi hawa pamoja na washitili wao. Mbali na hilo, kuna haja ya kuelimisha wananchi wetu kuwa macho na mali zao. Maana hazitaishi milele. Pia haina sababu wao waendelee kuishi kwenye umaskini wa kunuka wakati wageni wanakuja na kujichotea watakavyo.
Chanzo: Tanzania Daima J’tano kesho.
Tuesday, 12 September 2017

Kijiwe chafunga kumuombea Lissu

Barua ya wazi kwa maaskofu Kilaini na Nzigilwa

Image result for photos of kilaini na nzigilwa
          Wahashamu maaskofu Methodius Kilaini na Eusebius Nzigilwa,
            Kwanza, nawaamkua shikamooni; na kukwapa pole kwa majukumu yetu ya kiroho na kidunia. Pia nawapa pole kwa yaliyowakuta. Maana si madogo. Ni pale mlipotuhumiwa, kabla ya kukiri, kuchotewa fedha zilizotokana na kashfa ya wizi wa fedha za umma wa watanzania maskini ijulikanayo kama Escrow mlizopewa na mtuhumiwa na muasisi mkuu wa kashfa hii, James Rugemalira ambaye sasa yuko korokoroni akituhumiwa kwa makosa ya kulihujumu taifa na kuuibia umma. Hivyo, sitaweza kuingi undani wa suala zima tokana na sababu za kisheria na ukweli kuwa mnalijua vizuri hata kuliko mimi kama wanufaika ambao sasa wanajitenga na mshitili wao.
            Hivi karibuni, nilisoma tangazo lenu la tarehe 7 Septemba, 2017 kuutaarifu umma kuwa mmeamua kurejesha zile fedha kwa serikali baada ya kujiridhisha kuwa hazikupatikana kihalali. Je mmetubia dhambi hii itokanayo na uroho ambayo ni kinyume cha mafundisho ya Yesu Kristo? Je mmetumia vigezo gani hasa ikizingatiwa kuwa atoaye sadaka kanisani au matoleo, kama manavyoita, huwa haulizwi namna alivyochuma fedha atoazo? Maana ingekuwa hivyo, bila shaka mngelimuuliza Rugemalira alivytengeneza hiyo fedha kabla ya kuzichukua na kuishia kwenye kashfa ambao itawagharimu vilivyo kama mkondo wa sheria utafuata ikizingatiwa nyinyi ni viongozi na watumishi wa umma waliopokea fedha chafu zitokanazo na wizi wa fedha za umma. Je huu si ushahidi tosha kuwa hii fedha haikuwa ya kanisa bali yenu kutokana na kitendo mlichofanya mkidhani kitawasafisha kikaishia kuwafichua na kuwachafua zaidi?  Katika tangazo tajwa hapo juu, mnakiri kupokea fedha ambazo hamkutaja ni kiasi gani ingawa inafahamika ni shiling milioni 40 na ushei, hapo Februari 2014 kupitia kwenye akaunti zenu za benki.  Hii maana yake ni kwamba fedha tajwa ilikuwa benki kwa takriban miaka mitatu ikitengeneza faida. Je mmerejesha na interests zilizolipwa na benki tokana na kuwa na kiasi hiki kikubwa? Je tukiacha ubabaishaji na kujitetea, kweli kwenye nafsi zenu hamkujua kuwa fedha hii ilikuwa kubwa; na uwezekano wa mhusika kuipata visivyo halali ulikuwa mkubwa ikizingatiwa kuwa kashfa yake haikuanza jana wala juzi? Je mnategemea kufanikisha nini katika hatua hii ambayo kisheria ni ushahidi wa wazi unaoweza kutumika dhidi yenu? Je kwanini mlingoja mpaka Rugemalira akamatwe? Je angeendelea kunyamaziwa mngechukua hatua mlizochukua au ni baada ya kugundua kuwa mambo sasa si mchezo wala mazoea kama ilivyokuwa imezoeleka nchini ambapo mafisadi wakubwa walizoea kulindwa na kuengwaengwa huku wakiwakoga wale waliowaibia? Kuna haja ya kutubu na kujisuta sana huku mkisema ukweli ili mueleweke na ikibidi kusamehewa au kuhukumiwa kulingana na wenye fedha watakavyoamua.
            Wapendwa, naomba niendelee kuwadodosa lau ukweli ujulikane ili uwaweke huru.  Katika tangazo lenu mlidai kuwa fedha husika ilikuwa ni matoleo.Je kama kweli yalikuwa ni matoleo, kwanini yaliingizwa kwenye akaunti zenu na si kwenye akaunti za makanisa yenu? Hapa nani anasema ukweli; na utaratibu wa kupokea matoleo ni upi kwa mujibu wa kanuni za kanisa? Je kwanini mmeamua kurejesha fedha serikalini na si kwa yule aliyewapa au familia yake wakati mkijua serikali aihusiki kwenye kashfa hii? Je mlipata ushauri wa kisheria ua wa kidini katika kufikia hatua hii hatari. Kwani, kiushahidi wa mazingira, hamna tofauti na wanufaika wengine waliohongwa tokana na nafasi zao katika utumishi wa umma ambao nanyi, kama watumishi wa kiroho, mnahusika? Je kitendo chenu cha kupokea fedha chafu kwenye akaunti binafsi kinatoa funzo na picha gani kwa jamii yetu? Je mnadhani mlichofanya ni suluhu ya sakati hili linalopaswa kuisha kisheria?
            Wapendwa, japo sitaki niseme mengi wala kuhukumu ili nisihukumiwe, tangazo lenu limeficha mengi zaidi ya liliyoweka wazi. Kwa mfano, kwanini hamkueleza utaratibu unaojulikana kikanisa wa muumini kutoa matoleo kwa kanisa ili umma upime kama kilichofanyika ni sawa au si sawa? Je kwanini mmechukua muda mrefu kufikia uamuzi mliofikia? Lazima kuwe na sababu zaidi ya mhusika kuwa korokoroni. Je mlifanya jitihada za kumrejeshea aliyewapa hiyo fedha kabla ya kufikia kuzipeleka serikali au mnafanya hivyo, ili serikali na umma usiwashughulikie?
            Nimalizie kwa kusema kuwa kitendo chenu kinaacha maswali mengi kuliko majibu. Sidhani kama serikali itaona sincerity kwenye kitendo hiki zaidi ya kuwa mbinu ya kutaka kuepukana na matokeo ya kashfa hii ambayo ni kufikishwa mbele ya vyombo vya dola ili haki itendeke. Maana, hali tuliyo nayo nchini kwenye ufisadi inatisha na kukatisha tamaa ingawa rais anajitahidi kupunguza madhara na ukubwa wa tatizo ambalo watangulizi wake walililea na kulifumbia macho. Si viongozi wa serikali wala wa kiroho japo si wote, imewaozesha na kuwaharibu kiasi cha kusahau hadhi, heshima na wajibu wao kwa umma. Ushauri wangu wa bure kwenu ni kwamba kirini kukwa mlipotoka na muombe msamaha mambo yaishe ili liwe somo kwa wengine wanaodhani kuwa wanaweza kutumia nyadhifa zao kula na mafisadi.
Chanzo: Tanzania Daima J’pili leo.

Mlevi ataka Katiba Mpya kama Kenya

            Baada ya mwana wa mfalme U-freedom Kinyataa kunyang’anywa ulaji wa dezo unaosemekana kupatikana kiharamu kwa njia ya uchakachuaji ambao sasa umegeuka fasheni Afrika, ilibidi nisukuti. Tokana na kusukuti huku, leo sitaki longolongo wala mizungusho bali kusema kwa kinywa kipana tena kwa herufi kubwa kuwa kaya yetu inahitaji katiba mpya ili kufanya mambo kisasa na si kizamani kama ilivyo na ilivyozoeleka. Hebu msomaji tuseme pamoja kwa herufi kubwa “TUNATAKA KATIBA MPYA ILI TUFANYE MAMBO MAPYA”
            Naona yule anagwaya akidhani yatamkuta yanayowakuta akina Tunduni Liisu. Ogopa Mungu si miunguwatu. Wanaweza kufunga mwili wako lakini  si mdomo wako wala mawazo yako. Kwani kaya hii ni yao au mama zao? Hebu tusema pamoja “TUNATAKA KATIBA MPYA SASA VINGINEVYO HAPAKALIKI HAPA.”
            Japo inaweza kuonekana kuwa najipa ujiko na kujifagilia, ni kwamba mawazo yangu yamechangia kufikia hapa ninapoongelea. Naona yule anatikisa kichwa na kusonya. Kama unadhani hizi ni kamba au longolongo asome gazeti la Kenya linaloheshimika la Daily Nondo utakuta nondo na vimondo vyangu. Kwa wasiojua hawa jamaa wanavyopendana kiasi cha kutotaka wageni waingilie mambo yao, kupata fursa ya kutupa mawe mle si kawaida. Lazima kichwa kiwe kinajibu na kuchemka kweli kweli. Nadhani mimi ni mlevi pekee toka Bongo aliyepata fursa ya kutupa mawe mle si mara moja wala mbili. Naona yule anazidi kubeua midomo na kutikisa kichwa. Maskini hajui kuwa nabii hakubaliki nyumbani yaani kwa kilatini Nemo profita in patria sua. Hayo tuyaache.
            Kuna maswali ya kujiuliza. Je ilikuwaje mwana wa mfalme akanyang’anywa tonge mdomoni wakati alikuwa na kila zana za kuchakachua? Si baada ya kustukia mchezo wa uchakachuaji, mpinzani wake Jadwong Madwong amaye by extension ni rafiki yangu na dingi, akaenda kwa Pilato. Kwa vile Katiba ya kule inaruhusu kila mlevi kwenda kwa Pilato anapohisi hajatendewa haki si Pilato akampa alichotaka kwa kumpiga chini mwana wa mfalme. Just imagine. Unadhani ingekuwa Bongolala na katiba yetu viraka jamaa angetoboa kama wasemavyo huko? Wala kisingeumana.
            Kwa vile nimependa chesi hii, nawaalika walevi wote wapenda demokrasia bila ghasia na maendeleo vya kweli waje tupange namna ya kuwabana wanene wetu warejeshe Katiba yetu mpya ya jaji Jose Waryuba iliyouawa na majambazi na mafisadi ili wasinyee debe kama akina Singasinga na Rugetumbuliwa bila kumsahau jamaa yangu Manjilinji. Au vipi walevi? Semeni kwa pamoja ‘Tumechoka na longolongo, ubabaishaji na mauaji ya Katiba mpya ya kaya.” Sema tena “Tunataka Katiba mpya na si uongo mpya.”
            Ninapoandika hapa, dingi atakuwa akitabasamu kwa swahiba yake kupata fursa nyingine ya kujaribu urahisi huku ndugu yangu Eddie aliyeshabikia upande wa pili akiugulia kwa machungu ya hukumu hii takatifu.
            Tukirejea umuhimu na majaliwa ya Katiba mpya, lazima niseme bila kumung’unya kuwa huwezi kuendeleza kaya bila kuwa na haki na uhuru kwa wanakaya kama ilivyo sasa. Hivyo basi, wote wanoota ndoto za nchana kuwa kaya inaweza kuendelea kwa maigizo wanapoteza muda. Maana, Katiba mpya ndiyo muarobaini wa ufisadi, uvivu na ubabaishaji ambavyo dingi amejaribu kutumbua akaishia kuchoka kabla hata hajamaliza ngwe moja. Hata hivyo, amejitahidi. Sema angekuw anashaurika, hakuna jambo la maana angewatendea walevi kama kufufua nchakato wa Katiba mpya ili itumike kuleta usawa, haki na uwajibikaji kayani kama ilivyotokea kwa majirani zetu wa the country of man eat man hivi karibuni.
            Huwezi kuendeleza kaya wakati kuna matabaka ya walevi ambapo wapo wasioguswa na wanaotolewa kafara kwa sababu wanaeleza mawazo yao ambayo ni haki yao kikatiba. Huwezi kuendeleza kaya kwa katiba viraka na makengeza kiutendaji ambapo baadhi ya wahalifu wanakingiwa kifua tokana na ukaribu wao kwa wakubwa au ukubwa wa vyeo walivyoshika au kushikwa na maswahiba au waramba viatu wao kama ilivyo.
            Leo sichongi sana. Nakwenda kujiandaa kulianzisha la kudai upya katiba mpya. Kusema ukweli natamani Maraga angekuwa Bongo lau tumpe ofa na kumpongeza. Kwa wale wanaoatamia katiba yetu mpya wakae wakijua kuwa wanakalia kaa la moto. Kumbe naota! Hata hivyo, tuseme “TUNATAKA KATIBA MPYA.”
Chanzo: Nipashe J’mosi, jana.

Ama kweli aliyeko juu mngoje chini! Nani alitegemea tapeli Rugemalayer kulala Keko?

Mtuhumiwa na kingpin wa wizi wa IPTL James Rugemalira sasa ni mahabusu anayesota asijue atachomoka lini. Sawa na Hassy Kitilya, Sioi Sumari na vigogo wengine, anaendelea kuonja matunda ya jinai yake. Picha hii japo ni ya kiumbe anayeudhi, nimeipenda sana. Nadhani hili linapaswa kuwa somo kwa majambazi wengine ambao tawala zilizopita licha ya kulala nao kitanda kimoja ziliwaendekeza na kuwalinda kiasi cha kutukoga na fedha zetu. May they perish!

Ulimbukeni, umalaya na uoza kimaadili Magufuli aingilie

Wengi walimlaumu rais John Magufuli kusema wazi hataruhusu wasichana watakaopata mimba wasirejee mashuleni. Ushahidi kuwa Magufuli hana la kufanya zaidi ya kuwa na msimamo mgumu kama aliochukua ili kurejesha heshima ya taifa letu. Watoto wanaoshobokea ujinga toka Ulaya wanapaswa waadhibiwe vilivyo hasa wakati huu tunapopambana na mimba za utotoni na ukimwi. Wanaoruhusu majumba yao kutumika kufanyia ukahaba wanapaswa nao kuwajibishwa kwa kushitakiwa hata kutaifishwa nyumba na magari husika.

Government can still help teen moms

           Though President John Magufuli said it expressly–no pregnant girl will be allowed back to school under his rule; which’s logical–still the government’s the duty to make every effort to help such mas. After teen pregnancies playing hell with us, everybody’s wagging the tongue either in a hooray hoopla mood or agonisingly and negatively opposing this tough stance. However, there’ll be hell to pay in this hell of helluva as we play hell as a nation.  I know.  As a parent and a leader, Magufuli’s agonised just like anybody could. Again, if he steps in the shoes of the parents of gravid daughters, I’m sure the narrative will dramatically change. We need to think out of the box; understanding that, as the society, we’ve circumstantially contributed to creating this jumble either consciously or unconsciously through societal sloppiness, dishonesty, greed, selfishness, debauchery resulting from modernity, copycat behaviours and whatnots.
           If this stance isn’t being re-examined, its ramifications will be negatively immense to the future of the nation. For, it’ll increase ignorant and disadvantaged people in mothers and their unplanned children. Due to the challenging nature of school pregnancies, I think; we need to do the following:
               First, open adult education centers to cater for those who’ll drop out because of pregnancies or imbuing their colleagues. These centers must cater both for secondary and high school education for gravid girls; and their partners who happen to be students.  I can draw an example from Canada. Despite having all sorts of freedoms, such as teaching students that ngono is human rights, even Canada doesn’t allow teen mas to go on with schooling or curtail the development of the country and its citizens. Students kick up their heels as they like. However, they must see to it that they’re not becoming pregnant. The system here allows a person to complete his or her secondary education when he or she reaches 18. At this age whether pregnant or not anybody’s supposed to be in a class.   Anybody above 18 is entitled to complete his secondary school diploma at such adult education centers anytime he or she deems fit.
            Secondly, address the root causes. Although we tend to blame the victims, as the society, we’ve contributed to this anathema to our daughters.  For example, circumstantially, corruption’s a lot to do with pupil pregnancies.  How heavily do we punish perpetrators?  Thanks to corruption in upper echelons of powers, many citizens are ignorant and poor. You can see this in poor transportation, poor housing, and ill-equipped schools among others.
           Third, fight and eradicate systemic gender bias in which girls are condemned wholesale simply because they’re females. What are the traps and motivations that lure our girls into being impregnated? Are their families strong morally and materially? Why punishing girls only. What’s the position of the government which some pregnancies are caused by students? Will they still be eligible to proceed with studies while they actually are parents? What’s the punishment for adults say, teachers, or whoever impregnates a student? I’d argue that whoever impregnates a student, apart from being brought to book, must be jailed; and public employees who happen to win the case due to lack of watertight evidence or technicalities must be expelled from public services. This will send a strong signal to others still contemplating to do the same.
           Forth, seriously fight corruption and poverty which, in a sense, are the major causes of this beatinest challenge.
Lastly, amend or enact laws so as to hand down heavy punishments to perpetrators. For, they are robbing young girls of their lives. More important, we need to unequivocally address this problem making sure that anger and blame games aren’t used in addressing the problem.
Swahili’s it that when a baby poops on your hand, you don’t cut it nor do you throw the baby away.
Source: The Citizen Wed., today
Fear Nothing But Fear Itself